Matokeo ya awali yanaonyesha kuwa mgombea wa chama cha Democratic, Joe Biden anaongoza dhidi ya rais wa nchi hiyo, Donald Trump anayewania urais kupitia chama cha Republican
Leo Jumanne Novemba 3, 2020 vilio vilitawala katika uwanja wa shule ya Msingi Ibambila baada ya magari yaliyobeba miili ya wanafunzi wanne waliofariki kwa kugongwa na gari kuwasili.
Katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amesema chama hicho kimeongeza siku moja ya uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuomba kuteuliwa kuwania uspika na unaibu.
Zitto Kabwe anadaiwa kushikiliwa na Polisi alipokwenda kuwasalimia viongozi wa Chadema kituo cha polisi Oysterbay, lakini Kamanda wa polisi wa Kinondoni ameeleza kutokuwa na taarifa hizo.
Chama cha NCCR Mageuzi kimesema matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28, hayawezi kuhalalisha aliyeshinda na aliyeshindwa kwa sababu mchakato wa uchaguzi ulivurugika.