Seth Bosco ambaye ni mdogo wa marehemu Steven Kanumba, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumamosi baada ya kuzidiwa akiwa nyumbani kwa mama yake Mbezi jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania, Dk Harrison Mwakyembe amesema bunge lijalo atamwandikia barua Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ili atoe kibali kwa wabunge kuvaa batiki na vitenge wanapokuwa bungeni.