Ajali hiyo ilitokea Oktoba 24 eneo la mteremko wa Kumuyange wilayani humo baada ya basi la Emirates lililokuwa likisafiri kutoka Ngara kwenda Bukoba mjini kupinduka.
Wiki iliyopita, Tottenham ilitangulia kufunga mabao matatu na kuongoza 3-0 hadi dakika kumi za mwisho wakati West Ham waliposawazisha na mechi kuisha kwa sare ya mabao 3-3.
Ni wiki ya uamuzi. Ndivyo unavyoweza kuielezea wiki inayoanza leo wakati Watanzania milioni 29.2 watakapopiga kura kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wabunge na madiwani leshokutwa Oktoba 28.
Mahakama Kuu imeikazia kamba shule ya Eden ya jijini Mwanza kwa kutokuwasilisha michango ya watumishi wake katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), baada ya kutupilia mbali rufaa yake.
Miaka mitano ya Rais John Pombe Joseph Magufuli inaisha Jumatano. Ni siku tano tu toka hii leo. Tutatangaziwa rais atakayeunda serikali mpya. Suala la mitano tena au mitano kwanza, liko mikononi mwa wapiga kura wa nchi hii. Yes!