Waangalizi wa kimataifa kutoka taasisi ya EISA wamesema miongoni mwa kasoro zilizokuwepo katika uchaguzi ni wagombea kukamatwa na kuwekwa rumande na matumizi ya mabomu ya machozi.
Wakati mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad akisema hajui alipo naibu katibu mkuu wa chama hicho, Nassor Ahmed Mazrui ambaye tangu jana asubuhi Alhamisi Oktoba 29, 2020 hajulikani alipo, jeshi la polisi limesema linafuatilia suala hilo.