Chama cha NCCR Mageuzi kimesema matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28, hayawezi kuhalalisha aliyeshinda na aliyeshindwa kwa sababu mchakato wa uchaguzi ulivurugika.
Katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, thamani ya almasi ya rangi ya pinki ilipanda kwa asilimia 500, ofisa wa Rio Tinto, Sinead Kaufman ameiambia ABC.
Raia wa Tunisia ambaye aliua watu watatu kanisani nchini Ufaransa, amekutwa na maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya corona, Covid-19, jambo ambalo limechelewesha mahojiano, mtu aliye karibu na uchunguzi ameeleza.
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimewataka wananachama wake walio na sifa kuchukua fomu kuwania nafasi ya Spika na Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, mameya na wenyeviti wa halmashauri au manispaa.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema viongozi wa Chadema wamekamatwa kwa kuwa wamepanga kuongoza maandamano bila kutoa taarifa yoyote polisi.